Sheria Linganishi iliyojikwamua kutoka kwenye ukoloni
Mwaka wa 2019, Ralf Michaels (Mkurugenzi wa MPI) na Lena Salaymeh (École Pratique des Hautes Études - Paris Sciences et Lettres) walianzisha mradi wa utafiti wa ushirikiano wa muda mrefu juu ya sheria linganishi iliyojikwamua kutoka kwenye ukoloni (DeCoLa). Lena Salaymeh aliongoza programu hiyo pamoja Ralf Michaels hadi 2023. Kwamou Eva Feukeu ameratibisha mradi tangu 2022.
Sheria linganishi iliyojikwamua kutoka kwenye ukoloni hubainisha kwa mpigo hubainisha jinsi muundo wa usasa/hali ya ukoloni unavyoeneza uelewaji wa sheria na hutoa njia mbadala za kujikwamua kutoka kwenye ukoloni. (Hali ya ukoloni haimaanishi ukoloni tu, bali ni mtazamo wa jumla na wa ulimwengu wote wa fikra unaozingatia usasa.)
Sheria linganishi iliyozoeleka hutegemea dhana za kiepistimiolojia zinayotokana na muundo wa usasa/hali ya ukoloni na hii ina athari dhana kuu kadhaa au utendaji kazi katika sheria linganishi: kutumia nchi kama kitengo cha uchanganuzi, kupendelea sheria za kilimwengu juu ya sheria za kidini, kutazama. sheria ya kisasa kama bora kuliko mila ya kabla ya ukoloni na zilizopinga ukoloni. Kuondoa hali ya ukoloni kunalenga kushinda muundo wa pembezoni-katikati, kipengele muhimu cha usasa/ukoloni, kupitia dhana ya wingi, ikimaanisha uhalali wa mila nyingi na mpangilio wa kijamii.
Badala ya kupanga sheria linganishi kwa lengo la kuunganisha au "kusasisha" sheria, tunatetea kutumia sheria linganishi kuondoa mawazo ya kisheria na kuweka masharti ya wingi wa sheria. Uchanganuzi wa kujikwamua kutoka kwenye ukoloni unaonyesha hali ya ukoloni ndani ya sheria linganishi iliyozoeleka na hivyo kusaidia kuivuka.
Machapisho
Hapa kuna bibliografia iliyosasishwa mara kwa mara juu ya masomo ya sheria Linganishi iliyojikwamua kutoka kwenye ukoloni. Machapisho
Matukio
Taarifa juu ya matukio yaliyopangwa na yaliyopita utapata hapa.
Taarifa zaidi juu ya mradi huo